Katika hali ya kuhuzunisha, mwanadada mmoja aliyempa mpenzi wake figo ameelelzea kupoteza penzi hilo miezi kadhaa baadaye.

Kwa mujibu wa ‘The Mirror’ inaripotiwa kuwa Colleen Le, mwenye umri wa miaka 30, kutoka Marekani, alijitolea kumpa mpenzi wake figo yake moja baada ya kugunduliwa kuwa na maradhi mabaya ya figo.

Tatizo la figo zake lilianza alipokuwa na umri wa miaka 17, na aliarifiwa kwamba figo yake ingefanya kazi chini ya asilimia tano.

Baada ya kugundua kuwa ana uwezo wa kumpa, Colleen alitoa figo yake moja, na wote wawili wakapona kabisa Hata hivyo, uhusiano wao uliingia doa miezi saba baada ya upasuaji huo wakati Christian aliposema anataka kuhudhuria sherehe ya watu makapera mjini Las Vegas pamoja na marafiki zake wa kanisa.

Baada ya kurejea kutokea kwenye ziara hiyo, aliungama kwamba hakuwa mwaminifu kwake.

“Tulikuwa na mabishano mengi, hatimaye nilimsamehe na kumpa nafasi ya pili lakini baadaye tulitengana, Ikiwa tumekusudiwa kila mmoja wetu, Mungu atatuleta pamoja mwishowe,” Colleen alisema.

Katika kisa kingine cha namna hiyo, kwenye mtandao wa Tik tok, ilisambaa Video ambayo iliwavutia zaidi ya watu milioni mbili, huku wakimhurumia Jamaa mmoj alietemwa baada ya kutoa figo kwa mama wa mpenzi wake.

Kupitia video kwenye TikTok, Uziel Martinez alisema alikuwa amejitolea kumsaidia mama ya mpenzi wake wa zamani lakini alimtema na kuolewa na mwanamume mwingine.

“Nilitoa figo kwa mama yake, aliniacha na kuolewa mwezi mmoja baadaye, Sijambo, niko sawa kihisia, na nadhani na yeye. Sina chochote dhidi yake. tuko kwenye mahusiano mazuri,” alisema.

Mwanamume huyo kutoka Mexico alitupwa miezi michache baada ya kumpa mama ya mpenzi wake figo.

Young Africans kucheza CCM Kirumba
Rais wa Malawi afuta baraza lake la Mawaziri