Wanawake ni ‘maua’ ambayo yanapokuwa yamechanua vizuri hulifanya jicho la mwanaume kuganda kwa sekunde kadhaa ama kugeuza shingo kutoa ‘alama’ zake. Lakini kufanya hivyo ndani ya India kunaweza kukutia matatizoni.

Kamishna wa Kerala nchini India, Rishiraj Singh amewaacha watu midomo wazi baada ya kutangaza kuwa ni marufuku mwanaume kumuangalia mwanamke kwa zaidi ya sekunde 14 na kwamba atakayefanya hivyo anaweza kuishia jela.

Kamishna huyo alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipokuwa akizungumzia usalama wa wanawake nchini humo, kufuatia kuendelea kuripotiwa kwa matukio ya ubakaji.

Mbali na hatua hiyo, aliwashauri wanawake kujifunza mchezo wa martial art na karate kwa ajili ya kujilinda na kwa ajili ya afya zao. Aliwataka pia kuwa wanatembea na visu vidogo ili watakapovamiwa na wabakaji wajilinde.

Indian Womend karate

Kauli hiyo ilikosolewa vikali kwenye mitandao ya kijamii na kuzua ucheshi wa aina mbalimbali. Wengine walieleza kuwa amri hiyo ikipitishwa inaweza kuongeza soko kwa miwani ya jua kwa wanaume pamoja na saa za kwa ajili ya kuangalia muda wanapoangalia wanawake.

Hata hivyo, mwanasheria wa Mahakama ya Juu nchini humo, K V Dhananjaya leo ameiambia India Today kuwa kauli ya kamishna huyo haina mashiko kwani hakuna sheria yoyote nchini humo inayoeleza hayo.

“Hakuna kifungu chochote cha sheria ndani ya nchi hii kinachoeleza hayo na hakutakuwepo na kifungu cha kipuuzi cha aina hii katika nchi yoyote dunia,” alisema Dhananjaya.

Watumiaji wa mtandao wa Twitter wameipa hashtag ya 14secondsRule        (#14SecondsRule) wakishambulia kauli hiyo kwa vituko mbalimbali.

Waziri Wa Afya Ummy Mwalimu Akutana Na Balozi Wa Israel
Profesa Baregu: Tusimsingizie Nyerere kuhamia Dodoma, tutafute sababu za sasa