Usajili wa Mshambuliaji Kutoka DR Congo Heritier Makambo, umempa shaka mchambuzi wa Soka la Bongo Edo Kumwembe.

Makambo amesajiliwa Young Africans kwa mara ya pili na kutambulishwa rasmi kwa Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo mapema juma hili.

Kumwembe ambaye pia ni Mwandishi wa habari Mwandamizi ameonesha shaka katika usajili huo, alipokuwa akichambua usajili wa Young Africans kwenye kipindi cha Sports Arena cha Wasafi FM mapema leo Alhamisi (Agosti 05).

“Hizi ni hisia tu lakini Yanga walipaswa kujiridhisha kwanza kuhusu uwezo wa sasa wa Makambo. Ni yuleyule? Wana uhakika gani?”

“Wakishamaliza kujiridhisha kama ni yuleyule wajiridhishe tena na afya yake. Hana majeraha yoyote yaliyokwamisha kiwango chake huko alipo?”

“Nimeshtuka kuona mchezaji kama Fiston Mayele akitambulishwa kuwa mchezaji wa Yanga juzi bila ya kuonyeshwa picha wala video ambazo zingemuonyesha akipimwa afya.”

“Yanga walichoangalia ni rekodi zake tu nzuri za mabao kule DR Congo.” amesema Kumwembe.

Yanga hawakutaka sana kujihangaisha kwingine lilipofika suala la Makambo. Nadhani hawana mfumo mzuri wa kusaka wachezaji (scouting system). Wana uhakika gani kwamba wasingepata mchezaji mwingine hatari zaidi ya Makambo alivyokuwa kabla hajaondoka? Hawakutaka kujisumbua sana.

Chama: Ligi Kuu itakua ya 'MOTO' msimu ujao
Profesa kabudi awaonya watumishi wa Mahakama