Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma amesema kuwa kuna baadhi ya Wizara ni kichefuchefu kwani zimekuwa zikiongozwa na mawaziri mizigo.

Amesema kuwa kuna baadhi ya mawaziri mizigo ambao hata bajeti zao zimepata shida kupitishwa kutokana na utendaji kazi wao mbovu.

“Kuna Waziri hata nikifumba macho nikifumbua nikamuona nakimbia kutokana na utendaji wake wa kazi katika wizara anayoiongoza,”Amesema Musukuma

Aidha, Musukuma amewataja baadhi ya Mawaziri wanaozitendea haki Wizara zao kuwa ni Waziri, William Lukuvi wa Ardhi na Ummy Mwalimu wa Afya.

Hata hivyo, Musukuma ameongeza kuwa kuna baadhi ya Mawaziri wamekuwa wakifanya kazi kwa mihemuko ndio maana wao kama wabunge wanajitahidi kuwashauri wanapokuwa wameenda tofauti.

Madereva wanaovunja sheria kuswekwa mahabusu
Video: Sugu afichua mwanaCCM aliyemtembelea gerezani, Nyumba ya waziri yauzwa kwa mnada