Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Yustino Ndugai ameihoji Wizara ya Nishati kujua kama kuna mgao wa umeme nchini Tanzania.

Spika Ndugai amehoji leo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu kwa kikao cha asubuhi cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hoja hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Kilombero, Aboubakar Assenga kuhoji sababu za kukatika kwa umeme kila siku ya Jumanne Jimboni kwake.

Hata hivyo Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato ameliambia Bunge kuwa hakuna mgao wa umeme sehemu yoyote nchini Tanzania.

Mkutano wa tano wa Bunge la Jamhuri ya Muugano wa Tanzania umeanza jana tarehe 2 Novemba Jijini Dodoma na utadumu kwa wiki mbili hadi tarehe 12 Novemba.

Juventus kumrudisha Paul Pogba
Mmiliki jengo lililoporomoka Nigeria alicheza 'mchezo mchafu'