Kundi jipya la kigaidi linalojitangaza kuweka mizizi yake Afrika Mashariki linalojiita ‘Jahba East Africa’, limekula kiapo cha utii kwa kiongozi wa kundi la kigaidi linalojiita ‘Islamic State of Iraq and Syria (ISIS), Abu Bakr al-Baghdadi.

Kundi hilo lililoripotiwa kuundwa na wanamgambo wa zamani wa Al Shabaab inayoshirikiana na Al Qaeda kufanya mashambulizi ya kigaidi nchini Somalia na Kenya pamoja na nchi nyingine za Afrika Mashariki, limeendelea na kampeni ya kujiimarisha huku likikosoa utendaji wa Al-Shabaab.

Msemaji wa kundi hilo amekaririwa na mtandao wa ‘Site Intelligence Group na International Business Times wa Marekani akilaani Al Shabaab kwa madai kuwa imeshindwa kazi na imegeuka kuwa mfungwa wa kisaikolojia na kimwili.

“Sisi Jahba East Africa tunawashauri watu wote wa Afrika Mashariki kuachana na Al Shabaab na makundi ya wahisani wao kama Al-Mhajiroun, al-Hijra na Ansar Islam,” Msemaji wa kundi hilo anakaririwa huku akisisitiza kuwa kundi lao ni kundi tiifu kwa kiongozi wa ISIS.

“A new era will come to East Africa soon InshaAllah [God willing],” inasomeka tweet moja ya kundi hilo la Juhda East Africa.

Aliyemuua Osama Bin Laden akamatwa
Video Hii ya Simba aliyepambana na mafuriko Kenya yapata umaarufu