Ikiwa ni siku chache baada ya kundi wasanii Peter na Paul wanaounda kundi la P-Square kuripotiwa kutokuwa na mahusiano mazuri ugomvi wao unazidi kukua sasa mpaka kufikia hatua ya kuanza kutoa siri za ndani za kundi.

Paul wa P Square ametoa povu lake kwenye ukurasa wake ya Twitter kudai kwamba amefanya kosa kubwa sana katika maisha yake kwa kuitoa ngoma ya “Bank Alert” kuwa kama ya kundi.

Wengi tulikuwa tunafahamu kwamba wimbo wa “Bank Alert” ni moja ya ngoma za P Square, ila ukweli ni kwamba wimbo huo ulikuwa ni wa Paul, ila akaamua kuufanya kama wa kundi kwa kumuweka ndugu yake Peter.

Awali ugomvi wao uliripotiwa kutokana na madai ya Peter kusema kuwa inaonekana kuwa ndugu yake Paul hayupo tayari kuendelea kufanya kazi na yeye kwani ameweza kusitisha ziara yao ya US bila ya kuweka sababu yeyote.

Baadae walisuruhisha ugomvi wao lakini sasa mambo yakuwa tofauti baada ujumbe alioandika ya Paul katika ukurasa wake wa Twitter.

 

IGP Sirro amtumia ujumbe dereva wa Lissu, ‘inanipa tabu’
Mashabiki wa soka Zanzibar waushutumu uongozi wa ZFA