Mkongwe wa muziki, Daddy Showkey, ameliibukia bifu la wasanii mapacha waliokuwa wakiunda Kundi la P Square, Paul na Peter Okoye.

Ndugu hao waliokuwa wakisimamiwa na kaka yao, Jude Okoye, wameingia katika mvutano mara mbili tangu walipolianzisha kundi hilo mwaka 2013.

Kwa mara ya kwanza, walikorofishana mwaka 2012 kabla ya kufanya hivyo mwaka jana na hadi sasa hawajaweza kuwa pamoja.

Katika ujumbe wake kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Showkey alisema wasanii hao wanatakiwa kujua kuwa uhusiano mbaya walionao sasa unaweza kuhamia kwa watoto wao hapo baadaye.

“Fikirieni kuhusu watoto wenu, mnachokifanya kitabaki katika kumbukumbu ya watoto wenu…” aliandika veterani huyo.

Aidha kundi la Psquare lilivunjika kwa kile alichodai Peter kuwa pacha wake Paul hakuwa na heshima juu yake na familia yake na amewahi kusema kuwa kundi hilo linaweza likarudi endapo kutakuwa na heshima baina yao wawili ya ailimia 100 kwani hawezi kukubali kuona familia yake ikidharauliwa tena na ndugu yake huku aliahidi na kula kiapo kuilinda familia yake.

 

Bassogog arudishwa kikosini, Moukandjo akerwa na kustaafu
Wanawake kuwania Ballon d'or

Comments

comments