Mwanaharakati Kunje Ngombare  Mwiru, amezungumza mtazamo wake kuhusiana na sakata zima la msanii Wema Sepetu kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Amesema kitendo cha CHADEMA kumpokea Wema kinaonyesha dhahiri kwamba vyama vya upinzani vimeanza kupoteza mwelekeo kisiasa na vinashindwa kupambana na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kinashugulika na mambo mbalimbali yanayowakabili wananchi.

”Haiingii akilini kila mwenye tuhuma na kashfa akimbilie upinzani. Huo ni udhaifu mkubwa unaofanywa na viongozi wa vyama hivyo wameshindwa hoja za msingi kupambana na CCM sasa wana jisifu na kujigamba kwa kuwakaribisha watu wanaotuhumiwa, ”amesema Kunje.

Aliongeza kwa kusema ni jambo la kusikitisha na kushangaza kuona hata alipoingia Edward Lowassa CHADEMA, chama hicho kilikosa hoja na ndipo kilipoanza kupoteza mwelekeo na matokeo yake yameonekana katika uchaguzi mdogo, ambapo CCM ilipata ushindi mkubwa.

Kitendo cha CHADEMA, kupokea wanachama wenye tuhuma mbaya ni dhahili inaonesha chama hicho kinepoteza uelekeo na kukwamisha vyama vya upinzani.

Alimaliza kwa kusema wananchi wanapatwa na wasiwasi juu ya wanasiasa ambao ni watuhumiwa wa dawa za kulevya kuwepo kwao kwenye siasa ni kama maficho ya uhalifu.

 

Abracadabra Aiweka Kiporo Man Utd
Batuli ampinga Wema, 'Wasanii tulioshiriki kampeni za CCM tulilipwa na mikataba ipo'