Mashabiki watakao taka kupiga picha na staa wa filamu duniani Sylvester Stallone, maarufu kwa jina la Rambo watatakiwa kulipa zaidi ya millioni 2

Msanii huyo atahudhuria tamasha la mitindo (UK events) amablo litafanyika jijini London, Manchester na Birmingham Agosti na Septemba mwaka huu, mashabiki ambao wanataka kupiga naye picha lazima walipe pauni 849, ambazo ni sawa na 2,481,880 za Kitanzania.

Tofauti na kiasi hicho cha kupiga picha na msanii huyo mwenye umri wa miaka 72, tiketi zakiingilio kwanye tamasha hilo zitakuwa zinauzwa  pauni 125 hadi 325 sawa na 365,412 na 950,072 za Kitanzania.

Mashabiki wa msanii huyo wamechukizwa na kiwango cha fedha kilichowekwa kwaajili ya kupiga nae picha huku wengine wakidai kuwa inabidi wauze figo zao ili waweze kupata fedha za kupiga picha na staa huyo filamu

Mkali huyo wa flamu za kivita atahudhuria tamasha hilo la mitindo ikiwa nisehemu yake ya kukutana na mashabiki wake.

 

 

 

Pinda awafunda Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu
Malaysia: Shule zaidi ya 400 zafungwa baada ya wanafunzi kukosa pumzi

Comments

comments