Katika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika, Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimeiasa jamii na asasi za kiraia kufahamu kuwa ni jukumu la kila mmoja kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa watoto.

Hayo yamesemwa leo Juni 16, 2021 na Mkurugenzi wa TAMWA, Rose Reuben ikiwa ni siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambapo kauli mbiu kwa mwaka huu ‘Tutekeleze ajenda 2040, kwa Afrika inayolinda haki za watoto’.

“Katika kusherekea siku hii na kutazama juhudi za Serikali yetu katika kupunguza na kutokomeza kabisa vitendo vya ukatili kwa watoto na kuimarisha ulinzi wa mtoto, Tamwa tunatoa wito kwa jamii, asasi za kiraia kuweza kuona kuwa ni jukumu la kila mmoja kupinga kwa vitendo ukatili na unyanyasaji kwa watoto kwani malezi ya watoto yanaanzia katika ngazi ya familia,” amesema Reuben

Reuben amesema kulingana na kauli mbiu ya mwaka 2021  kamati ya wataalam ya Afrika kuhusu haki na ustawi wa mtoto wa Afrika ambapo Tanzania ni mwanachama na imesaini maazimio na makubaliano yenye vipengele 10 muhimu.

Pia amesema kuwa kila mtoto anufaike na elimu bora, kila mtoto alindwe kupitia vitendo vya kikatili na kutokutelekezwa, mtoto anufaike na uendeshwaji wa haki jinai za watoto katika mazingira yake, mtoto asishirikishwe katika maeneo ya migogoro na majanga na mtoto anapaswa kushirikishwa katika masuala yanayomuhusu.

TBS waanza ukaguzi wa magari nchini
Hakuna Hijja mwaka huu