Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini Kenya, Wafula Chebukati, amesema wapiga kura wenye ulemavu wa macho hawatapiga kura bila kusaidiwa kwani karatasi za kupigia kura hazitachapishwa kwa maandishi ya nukta nundu.

Jumamosi, Julai 17, Chebukati alisema kuwa watu wenye ulemavu wa macho watasaidiwa na maafisa wa IEBC waliohitumu ambao watakuwa katika kila kituo cha kupigia kura kote nchini Kenya wakati wa Uchaguzi Mkuu.

“Katika uchaguzi huu ujao, hatutakuwa na karatasi za kupigia kura zenye nukta nundu. Kama Tume, tumepiga hatua mbele, tuna nyenzo za elimu kwa wapiga kura katika maandishi ya nukta nundu,” Chebukati alisema.

Hatua hii ni tofauti na chaguzi za awali ambapo watu wenye ulemavu wa macho walikuwa wakisaidiwa na msaidizi ambaye alikula kiapo cha usiri kabla ya zoezi hilo.

Maafisa hao ambao watawasaidia katika zoezi hilo wamefanyiwa mafunzo kwa namna ambayo watafanya kura zao kuwa siri.

Hata hivyo, wakala atakuwepo ili kusikiliza kila kitu ambacho afisa msimamizi atamwambia mpiga kura kwa mfano, ni mgombea yupi angependa kumchagua.

Chebukati alibainisha kuwa IEBC ilifanya uamuzi huo kama juhudi za kujumuisha walemavu japo karatasi za kura za nukta nundu hazingepatikana kwa sababu hazikuwekwa kwenye bajeti.

“Tungependa kutambulisha karatasi za kura za nukta nundu katika chaguzi zijazo, lakini hatukuwa na bajeti ya wakati huu. Tutazingatia katika bajeti yetu na katika chaguzi zijazo,” Chebukati alieleza.

Wakati Huu Kulingana na ripoti ya utafiti ya Shirika la Afya Ulimwenguni ya 2021, kati ya watu milioni 39 wanaoishi na ulemavu wa macho dunian, 224,000 ni Wakenya na ripoti hiyo pia ilifichua kuwa Wakenya wengine 750,000, wanaugua matatizo ya kuona.

Rais amfuta kazi Mkuu wa Ujasusi
Wahudumu wa Afya waaswa maadili ya kazi