Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Alieu Momarr Njai, amesema kuwa matokeo ya awali katika jimbo moja lililothibitishwa na tume ya Uchaguzi nchini Gambia yameonyesha kwa rais wa sasa Adama Barrow anaongoza kwa kura kidogo.

Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwamba matokeo ya awali kutoka jimbo la kwanza kati ya majimbo 53 yalionyesha Barrow akiongoza kwa kura 657 dhidi ya 454 za mpinzani wake wa karibu Ousainou Darboe. 

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa leo Jumapili kwa kuzingatia mfumo rahisi wa wingi wa kura baada ya kuhesabiwa kutoka maeneo yote. 

Gambia inatumia mfumo wa kipekee wa upigaji kura kwa kutumia gololi zinazotumbukizwa ndani ya debe la kila mgombea ili kuepuka kura kuharibika. Gambi inatajwa kuwa taifa lenye kiwango kikubwa cha watu wasiojua kusoma na kuandika.

Gavana wa Talibani anusurika shambulio la bomu
Rais Samia afanya uteuzi