Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa amewapongeza Tanroads Mkoani Manyara kwa namna wanavyotekeleza wajibu wao kwa katika miradi ya barabara.

Amesema kuwa mara nyingi anafuatilia utendaji kazi wa wafanyakazi wa Tanroads na wamekuwa wanatekeleza miradi ipasavyo ikiwemo ujenzi wa barabara ya Babati-Kondoa.

“Pamoja na utendaji kazi wenu mzuri nitawaachia mawasiliano yangu ili mtu akiwa na jambo lolote tuweze kuwasiliana,” amesema Kwandikwa.

Aidha, kwa upande wake Meneja wa Tanroads Mkoani Manyara, Mhandisi Bashiri Rwesingisa amemshukuru Naibu Waziri huyo kwa pongezi hizo na kumhakikishia kuwa hawatabweteka.

Hata hivyo, mmoja kati ya katibu muhtasi wa Tanroads Mkoani Manyara, Ziada Yasini ametoa ombi kwa ajili ya kupatiwa ajira ya kudumu.

Samir Nasri kutumikia kifungo hadi Novemba mosi
Hospitali za serikali zaonywa kuwalipisha wajawazito, wazee na watoto