Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro amesema kuwa kwasasa yeye ni balozi wa Rais wa Jamuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na nchi yake.

Amesema kuwa ameridhishwa na kile ambacho Rais Magufuli anachokifanya kwa maslahi ya nchi na wananchi kwa ujumla.

Ameyasema hayo wakati akitangaza kujiuzulu nyadhifa zote ndani ya Chama Cha Wananchi (CUF), ambapo amesema kuwa kile ambacho walikuwa wakikipigania tangu awali kwasasa kina tekelezwa na serikali ya awamu ya Tano.

“Kama nilivyosema, kuanzia sasa mimi ni balozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nitamtangaza popote pale, iwe nje ya nchi ama ndani, siwezi kuendelea kutumikia chama, kwasasa lazima niwatumikie wananchi, kuna vijana wadogo wadogo tu, waliopo CCM wanawatumikia wananchi kwa vitendo, wanaacha alama, hata mimi nataka niache alama, nikumbukwe kwa kitu flani na si maneno matupu,”amesema Mtatiro

Hata hivyo, hapo jana Mtatiro alitangaza kujiuzulu nyadhifa zote ndani ya Chama Cha Wananchi (CUF) na kuomba kujiunga na chama cha mapinduzi CCM ili aweze kufanya siasa za maendeleo na si za porojo.

 

Habari Picha: Wananchi waendelea kupiga kura jimbo la Buyungu mkoani Kigoma
RC Hapi asmikwa rasmi kuwa Chifu wa Wahehe

Comments

comments