Klabu ya Real Madrid ipo tayari kutoa kiasi chochote cha pesa ili kumsajili kinda Kylian Mbappe kutoka AS Monaco kuchukua mikoba ya Karim Benzema.

Real wamemuona Mbappe kama mchezaji bora wa miaka ijayo na wangependa kumsajili mapema zaidi ili kuweza kuzipiku klabu mbalimbali barani Ulaya, huku taarifa zikisema tayari wameanza mazungumzo na AS Monaco juu ya Mfaransa huyo.

Kiwango cha Benzema kimezua maswali klabuni hapo kutoka na kushindwa kufanya kile bodi na mashabiki wanachotegemea hivyo kumuona Mbappe kama mkombozi huku wakiwa tayari kutoa kitita cha paundi 100 milioni.

Prof. Mbarawa kurudisha huduma za mizigo bandari ya kemondo
Gylfi Sigurdsson Kuondoka Liberty Stadium