Uongozi wa klabu ya LA Galaxy umeanza mipango ya kutaka kumsajili nahodha na mshambuliaji wa Man Utd Wayne Mark Rooney.

Gazeti la The Sun la nchini England, limeandika kuwa LA Galaxy wapo tayari kufanya hivyo kwa lengo la kuboresha kikosi chao ambacho kimekua kikifanya vyema katika ligi ya nchini Marekani (MLS).

Gazeti hilo limeongeza kuwa, uongozi wa klabu hiyo, pia upo tayari kuvunja rekodi ya malipo ya mshahara kwa kutambua Rooney ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa kwa mwaka.

Kwa sasa mchezaji anaelipwa mshahara mkubwa katika kikosi cha Galaxy ni kiungo na nahodha wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard.

Gerrard analipwa mshahara wa Pauni milioni 4 kwa mwaka, kiasi ambacho ni robo ya mshaha anaolipwa Rooney kwa akiwa Man Utd.

Rooney amekua na wakati mgumu wa kucheza katika kikosi cha kwanza cha Man utd, na tangu alipowasili meneja Jose Mourinho mshambuliaji huyo ameshindwa kufikia lengo hilo kwenye michezo sita.

Ligi Ya Taifa Ya Wanawake Kuzinduliwa Rasmi Mjini Dodoma
Michezo Ya Ligi Kuu 2016/17 Mwishoni Mwa Juma