Wasimamizi wa Ligi kuu ya soka nchini Hispania wanapanga kuanza kuziadhibu klabu ambazo zitaruhusu viti visivyo na mashabiki kuoneshwa kwenye runinga.

Hilo litaanza kutekelezwa kuanzia msimu ujao wa ligi ambao unatarajiwa kuanza mwezi wa nane (August).

Kanuni mpya zitazibana klabu za ligi kuu (La Liga) kuhakikisha maeneo yanayoangaziwa na kamera za runinga yamejaa mashabiki.

Lengo la hatua hii ni kuhakikisha viwanja vinavutia zaidi kwa watazamaji na pia kuongeza ushindani wa La Liga dhidi ya ligi kuu ya nchini England (EPL)

Mei 2015, Hispania ilipitisha sheria mpya za kuwezesha haki za kurusha michezo ya ligi ya La Liga na kuunganishwa na kuuzwa pamoja kama fungu moja.

Awali, klabu kama Real Madrid na Barcelona zilikuwa zikijitetea kivyake na kupata mikataba ya thamani kubwa.

Young Africans Walaani Figisu Figisu Za Angola
Tanzania Itasafa Sana Kuongezewa Uwakilishi CAF