Mshambuliaji wa FC Barcelona Lionel Messi La Pulga anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Argentina ambacho kitapambana na Hispania katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki mjini Madrid baadae hii leo.

Messi ambaye ni nahodha wa kikosi cha Argentina, hakuwepo katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Italia, ambao ulimalizika kwa mabingwa hao wa dunia wa mwaka 2006 kukubali kibano cha mabao mawili kwa sifuri katika uwanja wa Etihad mjini Manchester nchini England.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alishindwa kucheza mchezo dhidi ya Italia, kufuatia majeraha ya misuli ya paja ambayo yalikua yakimsumbua.

Kocha mkuu wa kikosi cha Argentina Jorge Sampaoli amesema, Messi amefanikiwa kufanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Hispania katika mpangilio mzuri kama alivyopangiwa na daktari, na amemridhisha kwa kuonyesha namna alivyo tayari kucheza hii leo.

“Kabla ya mchezo dhidi ya Italia, Leo alisema hatoweza kucheza kutokana na maumivu ambayo aliyahisi sehemu za paja, lakini alifanya mazoezi siku mbili kabla ya mchezo huo,”

“Kwa sasa yupo tayari kupambana kutokana na matibabu aliyofanyiwa na amethibitisha kuwa katika hali nzuri na katika mazoezi ya kuelekea mchezo wetu dhidi ya Hispania jambo hilo lilijidhihirisha” Amesema Sampaoli.

Hata hivyo Messi alizungumza na vyombo vya habari kabla ya mkutano wa kocha mkuu katika chumba cha mikutano cha uwanja wa klabu ya Atletico Madrid (Wanda Metropolitano stadium), na alieleza wazi kwamba yupo fit kucheza dhidi ya Hispania.

Hispania wanakwenda katika mchezo wa hii leo, baada ya kuambulia matokeo ya sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Ujerumani siku ya ijumaa, hatua ambayo imeendelea kuweka rekodi kwa kocha Julen Lopetegui ya kutopoteza michezo 17.

Bodi ya ligi yapangua mchezo mwingine
Nondo asimamishwa masomo UDSM

Comments

comments