Aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya Shirikisho la soka duniani FIFA, Dr Amos Adam yupo chini ya uchunguzi unaofanywa na kamati ya maadili ya shirikisho hilo.

Dr Amos Adam, ambaye ni raia wa nchini Nigeria, ameingia kwenye uchunguzi wa kamati ya maadili ya FIFA kutokana na kutuhumiwa kuvunja sheria za shirikisho hilo.

Hata hivyo taarifa ya kamati hiyo ya maadili haikuchimba kwa undani zaidi nini hasa kinachomuingiza mdau huyo kwenye uchunguzi huo, ambao unahisiwa huenda ukawa unahusiana na masuala ya ufisadi ambayo yamechukua nafasi kubwa kwa sasa.

Kama itakumbukwa vyema Dr Amos Adam, aliwahi kuwa mjumbe wa kamati kuu ya FIFA hadi mwaka 2010, baada ya kufungiwa  kujihusisha na masuala ya soka kwa muda wa miaka mitatu kutokana na kosa la kuomba mlungula ili kupiga kura ya kuchagua mwenyeji wa fainali za kombe la dunia.

Dr Amos Adam, alikuwa kiongozi wa juu katika serikali ya Nigeria kwa miaka 20, na alifikiriwa kuwa kati ya watu ambao wangemrithi Issa Hayatou katika nafasi ya urais shirikisho la soka barani Afrika (CAF).

Pamoja na kufungiwa miaka mitatu, pia alitozwa faini ya faranga za Uswiz 6341.

Dynamo Kiev Kusimamishwa Mahakama Ya UEFA
Wanawake Nao Wahimizwa Kukaa Mita 200