Skendo ya Rkelly bado ni changamoto kwa mwimbaji huyo nguli ambapo amejikuta akiwa mpweke kutokana na kila mtu kumkimbia hadi kufikia label yake kuwa mbali na muimbaji huyo

Taarifa kutoka  mtandao wa TMZ zimeripoti kuwa Label ya RCA Records imeamua kusimamisha kuachia ngoma za mwimbaji huyo hadi skendo yake ya unyanyasaji wa kingono itapomalizika

Chanzo cha karibiu cha mikataba ya Rkelly  pamoja na label ya RCA/Sony imesema label hiyo haitatayarisha wimbo wowote mpya kutoka kwa kellz, haitoweka pesa kwenye mradi wake wowote pia haitaachia wimbo wowote mpya  hadi skendo yake pamoja na shauri lilipo mahakamani mjini Atlanta Georgia  kumalizika.

Mwanamziki huyo bado anaidai RCA/Sony kwani hivi karibuni alikuwa anashinda studio kutengeneza muziki chini ya mkataba na anahitajika kuachiwa albamu mbili chini ya lebo hiyo.

Weusi wawajibu wasanii wa Kenya kampeni ya ‘Play Kenyan Music’
Masharti ya Travis Scott kutumbuiza fainali za Super Bowl 2019

Comments

comments