Siku chache baada ya Mtangazaji nguli, Gardner G. Habash kukihama kituo cha radio cha E-FM na kurejea Clouds FM kwa donge nono, aliyekuwa mkewe, Lady Jay Dee amekiongezea nguvu kituo hicho.

Jide ambaye kwa muda mrefu amekuwa katika mtafaruku na kampuni ya Clouds Media Group, ameonesha kupitia instagram kuwa ameamua kushirikiana na E-FM ambayo ingawa hajaeleza wazi kuwa ushirikiano wake utakuwa wa aina gani na ni kwa jambo lipi.

“jidejaydee#HuuMchezoHauhitajiHasira #NdiNdiNdi Efm feat Jide,” aliandika Jide.

#HuuMchezoHauhitajiHasira #NdiNdiNdi Efm feat Jide ???

A photo posted by Lady JayDee (@jidejaydee) on


Baadhi ya watu wameanza kuhisi mwimbaji huyo mwenye ukwasi na sapoti kubwa ya mashabiki anaweza kuwa amenunua kipande cha hisa za redio hiyo ambayo awali ilikubwa na tetesi kuwa huenda yeye ndiye mmiliki. Hata hivyo alizizima tetesi hizo baada ya kueleza kuwa yeye sio mmiliki wa wa E-FM.

Korea Kaskazini yajiandaa kufyatua bomu la nyukilia, Kusini yajipanga kujilinda
Makonda amkataa Mkurugenzi wa Jiji, abaini Wizi Mkubwa