Mwimbaji Judith Wambura, Maarufu kama Lady Jay Dee amevunja ukimya kufuatia sakata la aliyekuwa mumewe, Gardner G. Habash kumtolea maneno ya udhalilishaji na kejeli siku kadhaa zilizopita, yalizua sintofahamu.

Mwimbaji huyo amemuandikia barua Gardner yenye anuani ya ofisi anayoifanyia kazi hivi sasa ya Clouds Fm, akimtaka kuomba radhi ndani ya kipindi cha siku saba.

Barua hiyo ya Lady Jay Dee aliyoiandika kupitia mwanasheria wake, Aman G. Tenga imemtaka mtangazaji huyo kuomba radhi mbele ya umma ndani ya kipindi kilichotajwa.

Gardner anadaiwa kutoa kauli za udhalilishaji dhidi ya Jay Dee, tarehe 6 May 2016, alipokuwa akisherehesha tukio la kumtafuta Mrembo wa chuo cha TIA (Miss TIA 2016), lililofanyika DCS Park ambayo zamani ilikuwa ikiitwa TCC.

Moja kati ya masharti yaliyotolewa na Mwanasheria wa Jide linasomeka, “Kumuomba mteja wetu msamaha mbele ya umma (public apology) ili mteja wetu aridhike haraka iwezekanavyo.”

Inamueleza Gardner kuwa endapo atakataa kuomba msamaha ndani ya siku 7, atakabiliwa na hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwa kosa hilo.

Barua1Barua3Barua2

Lipumba alia na Rais Magufuli, adai ni chanzo cha sakata hili
AY, FA waivimbia Tigo Mahakama Kuu, Wapewa Tarehe ya kuvuna au kuchimba

Comments

comments