Mwimbaji Lady Jay Dee na mumewe wa zamani, Gardner G Habash wameurejesha upendo uliokuwa kati yao miaka kadhaa iliyopita, kabla ya vuguvugu la ugomvi uliovunja ndoa yao.

Hii imethibitishwa na kitendo alichokifanya mwimbaji huyo wa ‘Joto Hasira’, ambapo jana aliweka picha ya Gardner kwenye Instagram na kumtakia heri katika kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.

Jide alimuandikia ujumbe akimtakia heri hiyo ikiwa imechelewa (belated) huku akimpa heshima ya kumuita kwa majina yake yote matatu halisi.

Kupitia ujumbe huo, Jide ameawaonya wale wambao wataandika matusi huku akichombeza na maelezo kadhaa ya ucheshi na kupigia debe project yake ambayo hadi sasa hajaiweka wazi ya ‘I don’t Care’ (Sijali).

“Happy belated birthday Ndetaramo Fikirini Habash .  ONYO Kuweni na adabu kwenye hii post mkileta nye nye nye nye nye au matusi tu mnakula block ….. MATUSI = BLOCK ☹️ ☹️
#BingwaWaKujihami . ZINGATIA|Napokea zawadi kwa niaba ikiwemo miamala ya fedha taslimu kwenye number yangu ile ile , pamoja na vifurushi. Because #IDontCare 🙄 #Past  #NewPassport 😀😀 cc @1travela


Jide na Gardner walikuwa miongoni mwa ndoa za watu maarufu zilizokuwa na nguvu na mvuto kwa jamii nchini. Hata hivyo, ndoa yao iliingia doa na wawili hao wakatalakiana. Awali Gardner ndiye aliyekuwa Meneja wa mkewe.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 19, 2019
Spika Ndugai amvutia pumzi mbunge mwingine Chadema

Comments

comments