Nyota wa zamani wa mchezo wa Kikapu nchini Marekani Lamar Odom amefunguka majuto yake baada ya kuwahi kuukataa ushauri wa rapa Jay-Z.

Amesema kuwa kauli ya Jay-Z  ya kumkatalia kuanzisha Record Label, Lamar Odom alihisi ni fitna za Jay na kuwa anaogopa ushindani.

Amesema hayo katika kipindi cha In Depth with Graham Bensinger ambapo Odom ameeleza kuwa aliwahi kumfuata Jay-Z na kumwambia kwamba anataka kuanzisha Record Label kwa ajili ya kusimamia kazi ya msanii wake mmoja ambaye alikuwa anamkubali.

Jay-Z alipinga wazo hilo na kumtaka Odom ajikite kwenye biashara ya ‘Real Estate’ yaani biashara ya mali isiyohamishika kama majengo na ardhi, ni biashara ya kununua na kupangisha au kuuza vitu.

Aidha amekiri majuto hayo baada ya kukataa ushauri wa Jay-Z na mara baada ya kushindwa kufanya alichokuwa anataka.

Siku tatu za uboreshaji daftari la wapiga kura Dar
Maambukizi ya Corona Nchini China yazidi kupungua

Comments

comments