Beki kutoka nchini Ghana Lamine Moro amewaaga mashabiki wa soka nchini, baada ya kuthibitishiwa na uongozi wa Young Africans kuwa, hatokuwa sehemu ya kikosi cha klabu hiyo msimu ujao wa 2021/22.

Young Africans ilitoa taarifa kwa umma juzi Jumatano (Julai 28), juu ya kuachana kwa heri na beki huyo aliyewatumikia kwa misimu miwili.

Lamine Moro ameandika: Baada ya miaka miwili ya kuwa hapa Tanzania, napenda kusema ahsante kwa kilabu ya Young Africans SC (Yanga), wafanyikazi wake, mashabiki wa Yanga pamoja na Wachezaji wenzangu.

Pamoja tulipitia nyakati nzuri na nyakati mbaya. Lakini sisi tulisimama pamoja.Yanga Ni Klabu niliyopendezwa nayo na yenye utamaduni mzuri.

Imekuwa ni raha na heshima kuvaa jezi ya Yanga SC.Nitakumbuka kila wakati mda mabao nilikaa hapa Tanzania pamoja na ndani ya Yanga SC!

nawatakia kila la heri! Asante Tanzania Ahsante Yanga SC Asante sana

Serikali kuingiza US dola bilioni 2 mwaka 2025 kupitia mazao
Waziri Gwajima atoa maagizo haya kwa Mafamasia