Beki na Nahodha wa kikosi cha Young Africans Lamine Moro amesema ameshindwa kujua alichomkosea kocha mkuu wa klabu hiyo Nasreddine Nabi mpaka sasa.

Lamine alikataliwa na kocha huyo kujiunga na wachezaji wenzake kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kesho Jumamosi (Julai 03) dhidi ya Simba SC.

Moro amedai kuwa alipewa taarifa na uongozi wa Young Africans kuwa anatakiwa kuungana na timu ikitoka Tabora lakini akiwa anajiandaa kwenda kambini alipata ujumbe kuwa hatakiwi kwenda kambini kwani hayupo kwenye mipango ya mchezo dhidi ya Simba SC.

“Mpaka sasa sifahamu nini nimemkosea Kocha, amenizuia kuwa kambini kwa ajili ya kujiunga na wenzangu kuelekea mchezo na Simba SC.”

“Nakosa pakushika kwa maana viongozi walinitaka nijiunge na wenzangu kambini lakini baadae nikapokea taarifa iliyonitaka kutokwenda huko kwa madai sipo katika mpango wa mchezo dhidi ya Simba SC.

Lamine Moro alikumbwa na kadhia hiyo sambamba na kiungo kutoka nchini Rwanda Haruna Niyonzima, ambaye naye ameshangazwa na maamuzi ya kutotakiwa kambini.

Lissu aeleza siku atakayorudi Tanzania, atakachofanya
Nugaz: Simba waache 'JANJA JANJA' tucheze mpira