Meneja wa Muda wa Chelsea Frank Lampard amesema, Mason Mount, atasaini mkataba mpya na Chelsea “katika ulimwengu mzuri” lakini akakubali hali inaweza isiwe rahisi kwa kiungo huyo wa kati wa Timu ya Taifa ya England.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anakaribia kuingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake na amekuwa akihusishwa na kuhama katika klabu hiyo aliyojiunga akiwa na umri wa miaka sita.

Pande hizo zimekuwa katika mazungumzo kwa muda mrefu wa msimu huu kuhusu mkataba mpya lakini zimeshindwa kufikia makubaliano na inaonekana kuna uwezekano mkubwa ataondoka huku Liverpool na Manchester United wakiripotiwa kumtaka.

Ikiwa hakuna nyongeza iliyokubaliwa itamaanisha yuko huru kuanza kufanya mazungumzo na klabu nyingine mwanzoni mwa mwaka ujao, lakini Chelsea wanaweza kutafuta kumuuza msimu wa joto ili kuepusha uwezekano wa mhitimu huyo wa akademi kuondoka bure.

Lampard, ambaye alimpa nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza, Mount mwaka 2019 na mara kwa mara amekuwa akitoa pongezi kwake, alisema klabu lazima ifanye kazi kuwaonyesha wachezaji wa akademi kuna njia ya kuelekea upande wa wakubwa bila kujali mustakabali wa Mount.

“Ni jambo gumu kwangu kulizungumzia kwa sababu siko ndani ya kichwa cha Mason na kwa mtazamo wa  klabu,” alisema Lampard. Kwa maana ya vitendo ni katiya pande zote mbili. Sishangai kwa sababu hili ni soka.

Je! kila mtu anajua ninampenda sana Mason Mount kama mchezaji wa mpira? Ndiyo, hakika, bila shaka.

Simba: USM Alger wanafungika kirahisi
Young Africans hawatanii fainali ya CAF