Nuru imewawakia wachezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza kwani siku chache baada ya Steven Gerrard kuteuliwa kuwa kocha wa klabu ya Rangers inayoshiriki ligi kuu nchini Scotland, klabu ya Derby County imemtangaza kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Chelsea, Frank Lampard kuwa kocha mpya wa klabu hiyo.

Derby County imefanya uamuzi wa kumteua Lampard mwenye umri wa miaka 39 na kumpa mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo ikiwa ni wiki moja baada ya kuondoka kwa kocha Gary Rowett.

Mwenyekiti wa Derby County, Mel Morris amesema anafurahia kuwa na kocha aina ya Frank Lampard kwani ni mshindi na anajua ni kitu gani anatakiwa kufanya ili kupata mafanikio. Morris ameongeza kuwa amekuwa na mapenzi na Lampard kama mchezaji na akiwa nje ya uwanja.

Kwa upande wa Lampard amesema ni jambo la kipekee kwake kupata kwani amekuwa akitamani kupata nafasi ya kuwa kocha wa timu yenye utamaduni na historia kubwa kama Derby County.

 

 

 

Tafiti: Kila baada ya sekunde 6 watumiaji wa tumbaku hufariki dunia
Hii ndo timu atayohamia Lionel Messi akiondoka Barcelona