Mshambuliaji wa klabu bingwa nchini England Chelsea Loic Remy huenda akaihama klabu hiyo kabla ya dirisha la usajili halijafungwa mwishoni mwa juma hili, kufuatia mipango inayosukwa na viongozi wa Las Palmas ya Hispania na Cagliari ya Italia.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, msimu uliopita alipelekwa kwa mkopo Crystal Palace, lakini hakufanikiwa kufikia lengo baada ya kucheza michezo minane pekee.

Baada ya msimu wa 2016/17 kumalizika, Remy alirejea Stamford Bridge na kujumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 25 waliofanya ziara ya kujiandaa na msimu mpya nchini China na Singapore, lakini mpaka sasa hajabahatika kuwa sehemu ya vikosi vilivyocheza michezo mitatu ya ligi ya England.

Alijiunga na Chelsea mwaka 2014 akitokea Queens Park Rangers kwa gharama ya Pauni milioni 10.5.

Rais aagiza polisi kuwaua wanaogoma kukamatwa
Lissu apingwa, atakiwa kutoigeuza TLS kama taasisi yake binafsi