Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (Latra CCC) limependekeza nauli za abiria kwa treni ya mwendokasi (SGR) kutoka mkoa ya Dar es Salaam hadi Dodoma Sh19, 000 kwa watu wazima na wadogo Sh9, 000 kwa daraja la kawaida.

Akizungumza Dar es Salaam leo Desemba19, 2022 kwenye mkutano wa kujadili mapendekezo ya nauli zilizowasilishwa na wadau juu ya usafiri huo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Latra CCC, Leo Ngowi ameishauri Latra kutokuidhinisha kutumikia mapendekezo ya TRC kwani hazikuzingatia uhalisia wa vipato vya maisha ya Watanzania.

“Tunashauri Latra wasiidhinishe kutumikia viwango hivyo vya nauli na badala yake nauli ziwe chini ya Sh8, 000 Ili kuvutia abiria wengi zaidi na kuleta maana halisia ya lengo la kuwa na mradi wa Reli ya kisasa (SGR),” amesema Leo.

“Viwango tuliyopendekeza tulijadili na kufanya tathimini Kwa kuzingatia mataifa mengine yaliyoanza kutumia usafiri huo ikiwemo Kenya, India, Uingereza bei zao ziko chini na serikali zao hutoa ruzuku kupunguza makali ya nauli kwa wananchi wake,” amesema.

Wakati huo nuali ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro limependekeza Sh8, 000 kwa watu wakubwa na watoto Sh4, 000.

Viwango hivyo vinakuwa tofauti na vile vilivyowasilishwa na kupendekezwa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra), kwamba nauli ya kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa daraja hilo Sh59, 494 na kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro Sh 24, 794.

Naye Frederick Massawe Kaimu Mkurugenzi wa biashara wa TRC, amesema walipanga viwango hivyo kwa kuzingatia fedha ya uwekezaji uliofanyika na uweze kujiendesha.

“Lazima tuangalie huduma za abiria na mizigo, shirika tumeangalia gharama za uendeshaji miundombinu, utengenezaji na kuangalia namna ya kurudisha fedha iliyotumika ya wananchi ili kupunguza gharama za Serikali,” amesema Massawe.

Hata hivyo, Mtendaji Mkuu wa Latra, Habibu Saluo amesema bado wanaendelea kupokea maoni na wanafanya hivyo ilikupata maoni mengi yatakayowasaidia kufanya maamuzi sahihi.

“Unajua tulichokifanye leo ni kuwaita TRC kiwango walichokipendekeza wakiseme mbele ya wadau na tusikilize wadau watasemaje kabla ya kuja na viwango halisi,” amesema Saluo.

Dkt Mabula atoa maagizo haya kwa wakurugenzi, makamishna wa ardhi wasaidizi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 20, 2022