Serikali, imeiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA), kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kukaa pamoja na kupitia idadi ya magari madogo yaliyopewa leseni za usafirishaji wa abiria, yanayokiuka masharti ili kuwachukulia hatua madereva na wamiliki.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini kupitia taarifa yake aliyoitoa kwa waandishi wa Habari Julai 22, 2022 na kusema Jeshi la Polisi linapaswa kufanya operesheni zitakazosaidia ukamataji wa magari yanayoendeshwa kwa kukiuka taratubu za kisheria.

“Madereva wote wanaoendesha vyombo vya moto vinavyotembea Barabarani kwa kukiuka sheria kuvunja sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria ili kupunguza ajali za barabarani,” amesema Naibu Waziri Sagini.

Muonekano wa Barabara iliyoboreshwa.

Amesema, Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani na mamlaka zote zinazohusika wanatakiwa pia kuendelea kutoa elimu kwea abiria na kushauri kutumia usafiri wa mabasi au vyombo vingine vya usafiri vilivyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya vyombo vya moto kwenye barabara zilizoboreshwa nchini, huku hali ya usalama barabarani ikiwa ni ya kuridhisha huku Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau wamekuwa wakihimiza makundi mbalimbali yanayotumia barabara kuwa makini kwa usalama wao pamoja na mali zao.

Uboreshaji wa Miundombinu ya Barabara kuu za Mikoa, Wilaya na Vijijini nchini.

Wawili wauawa tukio la ujambazi wa kutumia Silaha
IGAD yaonya ujio wa baa la njaa Africa