Mipango wa klabu za Arsenal na Tottenham Hotspurs zote za jijini London, wa kumuwania Mshambuliaji kutoka nchini Argentina na klabu ya Inter Milan ya Italia Laurato Martinez, imegonga mwamba.

Klabu hizo ambazo zina upinzani wa jadi, zilitajwa kumuwania Mshambuliaji mwenye umri wa miaka 24 wakati wa usajili wa majira ya kiangazi mwaka huu 2021.

Laurato amesitisha mpango wa klabu hizo, baada ya kukubali kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Inter Milan, ambapo katika mkataba huo mpya hakuna kipengele cha kuruhusiwa kuondoka.

Kwa sasa usajili wa Martinez utakuwa mgumu kutokana na kukubali kuongeza mkataba mwingine, ambao utamuweka na kufungumana na klabu kwa muda mrefu kukiwa hakuna kipengele kitakacho muwezesha kuondoka.

Martinez alikuwa ana thamani ya pauni milioni 55, wakati akiwa amebakisha miaka miwili katika mkataba wake kwenye dirisha la usajili lililopita.

Kwa sasa thamani yake itapanda zaidi kulingana na mkataba, ambao atakwenda kutia kusaini, ingawa bado haijawekwa wazi ni lini, lakini imesemwa ni siku chache zijazo.

Coutinho atabiriwa mazito FC Barcelona
FC Barcelona yafichua siri