Aliyekua mkuu wa benchi la ufundi la mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG, Laurent Blanc anafikiriwa kuwa meneja mbadala wa Frank De Boer ambaye huenda akatimuliwa kazi mwanzoni mwa juma lijalo.

Uongozi wa klabu ya Inter Milan upo katika mipango ya kumsaka meneja mpya kutokana na kuchoshwa na mwenendo wa kikosi chao, ambacho tayari kimeshapoteza michezo minne ya ligi kati ya tisa waliyocheza mpaka sasa huku wakiambulia matokeo ya ushindi mara tatu na kupata sare mara mbili.

Jina la Blanc linatajwa kuwa miongoni mwa wakufunzi wanaopewa kipaumbele cha kuchukua benchi la ufundi klabuni hapo, kutokana na mafanikio aliyowahi kuyapata akiwa na PSG.

Blanc pia aliwahi kupita Inter Milan kama mchezaji kuanzia mwaka 1999 hadi 2001 kabla ya kutimkia Man utd na baadae alitangaza kustaafu soka mwaka 2003.

Guardiola Aridhia Kumtoa Sadaka Silva, Amuhusudu Julian Weigl
Rais Magufuli aongoza kwa kishindo kinyang’anyiro cha tuzo ya Forbes