Beki kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Arsenal, Laurent Koscielny, amekiri kuhisi ufahari mkubwa katika maisha yake ya soka, baada ya kuvaa kitambaa cha unahodha kwa mara ya kwanza katika ligi ya soka nchini England akiwa na The Gunners.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, alimpa unahodha beki huyo, wakati wa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita ambapo The Gunners walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Bournemouth.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 30, amewahi kukiongoza kikosi cha Arsenal kama nahodha wakati wa mchezo wa kombe la FA dhidi ya  Sunderland ambao walikubali kufungwa mabao matatu kwa moja.

“Ni fahari kubwa, ilikuwa mara ya kwanza katika michezo ya ligi, tayari nilikuwa nahodha katika FA Cup dhidi ya Sunderland na kisha Burnley, lakini heshima hii haikuniongezea presha, hii itabaki kuwa kumbukumbu muhimu katika maisha yangu ya soka,” alisema.

Shilole awahubiri mabinti
Ramires Ajiunga Rasmi Jiangsu Suning