Mshambuliaji kutoka nchini Serbia, Lazar Markovic ameshindwa kujizuia na kujikuta akifunguka kwa kusema kilichomuondoka Liverpool mwanzoni mwa msimu huu na kupelekwa kwa mkopo nchini Uturuki.

Markovic, ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Fenerbahçe na tayari ameshacheza michezo minne, amesema kuondoka kwake Liverpool hakukutokana na maendeleo ya klabu hiyo kama ilivyoelezwa katika vyombo vya habari, bali ni chuki binafsi ambazo zilijengeka kati yake na meneja aliyetimuliwa klabuni hapo Brendan Rodgers.

Markovic, amesema Rodgers alikua mtu wake wa karibu baada ya kumsajili huko Anfield mwanzoni mwa msimu wa 2013-14 akitokea kwenye klabu ya Benfica ya nchini Ureno, lakini hali ilikua ikibadilika siku hadi siku na ndipo alipobaini jambo ambalo lilikua limejificha kati yake na mtu huyo kutoka Ireland ya kaskazini.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, amebainishwa kwamba Rodgers alikua anampa afasi finyu ya kucheza, na mpaka sasa hajui ni kwa sababu gani.

Kuhusu ujio wa meneja mpya ndani ya Liverpool, Marcovic amesema anaamini huenda ukawa ni ukombozi kwake kutokana na sera ya Jurgen Klopp kuaminis ana vijana.

Amemsifia meneja huyo ambaye aliamua kujiweka pembeni baada ya kuiopa mafanikio klabu ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani, kwa kusema ana kila sababu ya kuifikisha mbali The Reds kama inavyotarajiwa na mashabiki wengi duniani kote.

Wanawake Nao Wahimizwa Kukaa Mita 200
Idadi Ya Wanaohama Mtwara Kuhofia Vurugu Baada ya Uchaguzi Yaongezeka