Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amesema wizara imepiga marufuku mikusanyiko yote isiyokuwa ya lazima ikiwemo ya kidini na siasa, mpaka pale itakapotoa maelekezo mengine na endapo ikihitajika kufanyika mkusanyiko itabidi kitolewe kibali maalum. 

Amesema hayo leo Julai 25, 2021 na Prof. Abel Makubi wakati akizungumza na vyombo vya habari amegusa maeneo mbalimbali ikiwemo daladala, misiba, matamasha ya muziki na michezo.

“Misiba yote ibada isizidi dakika 30 mpaka saa 1 na wahudhuriaji wawe wachache, hatujazuia kukaa misibani lakini mzingatie taratibu ikiwemo uvaaji Barakoa, unawaji mikono na kukaa umbali wa mita moja.”amesema Prof. Makubi

“Daladala zote zipakie ‘Level seat’ isipokuwa zenye nafasi kama mwendokasi abiria wasimame mbalimbali wapeane nafasi huku wakiwa na barakoa, lakini pia Bodaboda haitoruhusiwa kupanda mishikaki” amesema Prof. Makubi

“Mahabusu wote wanaoingia gerezani kwa mara ya kwanza au mtu aliyehukumiwa lazima apimwe kabla ya kuingia gerezani, lakini pia ndugu watakaokwenda kusalimia magerezani ataingia mmoja mmoja” amesema Prof. Makubi 

Simba SC Bingwa Kombe la Shirikisho 2021
Duchu kuondoka Simba SC