Mziki wa Tanzania unazidi kusonga mbele na kufika nchi mbalimbali zikiwepo nchi za magharibi na wasanii mbali mbali wakionekana kung’ara zaidi na kupata michongo tofauti tofauti kama kupata tuzo za kimataifa, wengine wakipata nafasi ya kusaini mikataba na makampuni makubwa ulimwenguni kusimamia kazi zao.
Wakati harakati hizo za kufanya mziki ufike mbali zikiendelea tumeanza kuona mabadiliko ya wasanii wanaofanya vizuri wakitaka kusaidia wasanii wenzao kwa kutumia Lebo ambazo zitawasimamia wasanii hao wadogo .
Siyo jambo la ajabu kuona msanii aliyetoka kimuziki kumsaidia msanii mwenzake au kumsimamia msanii mwenzake ili aweze kufanikisha ndoto zake kwani hata wasanii wanaotajwa kuwa wakubwa duniani nao pia wanasimamiwa na wasanii wenzao mfano Rihana, Kanye West na wasanii kibao wanasimamiwa na lebo ya Jayz inayokwenda kwa jina laRoc Nation.
Kibongo bongo tukio la kuanzisha lebo limeanza kuonekana kama kutaka kuzoeleka hapa nchini. Msanii kumsimamia msanii mwenzake halijaanaza leo, Madee alimsimamia Dogo janja, baadae wakaja Wasafi chini ya diamond platnumz, PKP chini ya Ommy Dimpozi, The Industry chini ya nahreel na Aika, leo pia Darasa katambulisha yake kwa Ufupi inayokwenda jina la CMG na hivi karibuni Mwana dada anaefanya poa na wimb wa Niroge alisema tutegemee japo siyo kwa sasa Mdee Music Lebo.
Swali ni je, Lebo hizi zipo kwa ajili ya kukuza muziki wa tanzania?
Leo msanii Darasa ametambulisha lebo yake ambayo atashirikiana kwa ukaribu kabisa na mtayarishaji wa video anayefanya vizuri nchini Hancana, huu utakuwa mwanzo mzuri kwa wasanii chipukizi ambao watapata bahati ya kusimamiwa na uongozi huo, lakini je zitakuja lebo ngapi kama hizi baada ya miaka 5?
Nawaza kwa sauti hivi kama kweli wasanii wetu wana lengo la kufanikisha na kufikisha mziki huu mbali wangeunganisha nguvu zao kwa pamoja na kutengeneza lebo chache zenye nguvu nchini badala ya kuanzisha lebo changa kila siku ili kutengeza ushindani wa kibiashara.