Mabingwa wa ligi ya England msimu wa 20105/16 Leceister City wamefanikiwa kumsajili kumsajili nahodha wa klabu ya Sevilla ya Hispania, Vicente Iborra kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 12.

Iborra mwenye umri wa miaka 29 amejiunga na Leceister City kwa mkataba wa miaka minne baada ya kufuzu vipimo vya afya.

Leceister City wameamua kumsajili kiungo huyo kutoka nchini Hispania, ili kuiongezea uimara safu yao ya kiungo ambayo imekuwa ikipwaya tangu kuondoka kwa Mfaransa, NG’olo Kante aliyejiunga na Chelsea mwezi Julai mwaka jana.

Iborra ameiacha Sevilla akiwa ameisaidia kutwaa ubingwa wa michuano ya Europa League mara tatu huku akifanikiwa kuitumikia klabu hiyo jumla ya michezo 169 tangu aliposajili wa mwaka 2013 akitokea Levante.

Iborra anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na Leceister City katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi barani Ulaya, akitanguliwa na beki wa kati, Harry Maguire aliyesajiliwa kwa Pauni milioni 17 akitokea klabu iliyoshuka daraja Hull City.

Bradley Lowery afariki dunia
Video: Saida Karoli alivyoonyesha uwezo wake akitimiza miaka 15