Vinara wa ligi kuu ya soka nchini England, Leicester City wameendelea kujizatiti kileleni, kufuatia ushindi wa bao moja kwa sifuri waliouvuna usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya Newcastle United.

Lecester City, wamevuna ushindi huo katika uwanja wao wa nyumbani, huku wapinzani wao Newcastle United, wakiwa chini ya meneja mpya Rafael Benitez, ambaye amechukua pahala pa Steve McLaren

Mshambuliaji kutoka nchini Japan, Shinji Okazaki, alifunga bao pekee na la ushindi kwa wenyeji katika dakika ya 25, na kuifanya Leicester City kufikisha point 63 katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini England.

Ushindi huo uneiwezesha Leicester City, kukaribia taji la nchini humo ambalo kama watafanikiwa kulichukua, itakua ni mara yao ya kwanza katika historia ya klabu hiyo ambayo ilizaliwa mwaka 1884.

Kabla ya mchezo huo, meneja wa Leciester City, Claudio Ranieri alikataa kukubali kwamba ndio wanaopigiwa upatu kushinda taji ligi, na badala yake alisisitiza kuwa lengo lao ni kufuzu kwenye michuano ya Europa League.

Michezo iliyowalia kwa Leicester City, hadi mwishoni mwa msimu huu,

Jumamosi 19 Machi 2016

Crystal Palace v Leicester 18:00

Jumapili 3 Aprili 2016

Leicester v Southampton 16:30

Jumapili 10 Aprili 2016

Sunderland v Leicester 16:30

Jumapili 17 Aprili 2016

Leicester v West Ham 16:30

Ligi Ya ZFA Pemba Kuanza Hii Leo
Esther Bulaya azidi kumtesa Wassira