Beki wa timu ya taifa ya Ghana, Daniel Amartey anakaribia kujiunga na klabu ya Leicester City ambayo inashiriki Ligi Kuu ya England.

Hatua hiyo imekuja baada ya klabu ya Amarte Denmark FC Copenhagen kukubali kumuuza kwa Leicester ambayo ipo katika kilele cha igi ya nchini England .

“Ni miongoni mwa mipango yetu kama klabu kuwakuza wachezaji hadi kiwango ambacho kinavutia timu nyingine kutoka katika Ligi kubwa ambazo huwanunua kwa kitita kikubwa cha fedha,” alisema kocha wa klabu hiyo, Anders Horshlt.

Amartey ambaye ameichezea FC Copenhagen mechi 63, anatarajiwa kuingia makubaliano binafsi na Leicester kabla ya mkataba wake kuidhinishwa.

Philipp Lahm Atamani Mazuri Zaidi Kutokwa Kwa Guardiola
Arsene Wenger Avunja Ukimya Kuhusu Game Ya Stoke City