Mabingwa wa soka nchini England, Leicester City wameandaa mabasi manne ya wazi kwa ajili ya sherehe za kutembeza kombe la ubingwa wa EPL, katika mitaa mbali mbali ya mji wa Leicester baada ya kumaliza msimu hapo jana.

Leicester City, ameandaa kufanya sherehe hizo huku wakiwa na kumbu kumbu ya kulazimika matokeo ya sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge hapo jana.

Mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Richard Monk amesema wamefanya maamuzi ya kuwa na mabasi manne ya wazi, ili kutoa nafasi kwa mmoja wao kujumuika na wachezaji ambao watakua na furaha ya kipekee katika shughuli hiyo.

Monk amesema wachezaji watapanda moja ya mabasi waliyoyaandaa sambamba na meneja Claudio Ranieri, na mengine yatawachukua maafisa wengine ambao walisaidiana na viongozi kukamilisha jambo hilo la furaha ambalo limeweka historia kubwa klabuni kwao.

Wenger: Nipo Tayari Kupambana Katika Soko La Usajili
Madee adai kuishi na Dogo Janja ni Kutimiza ndoto ya mpenzi wake aliyefariki

Comments

comments