Mabingwa wa soka nchini England, Leicester City wamenadi kumuweka sokoni mshambuliaji wao hatari Jamie Vardy, baada ya kutangaza thamani yake kuwa ni Pauni milioni 20.

Leicester City, wameanika wazi thamani ya mshambuliaji huyo kutokana na makubaliano yaliopo kwenye mkataba wake ambao unaendelea kumuweka King Power Stadium.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, amekua akiwindwa na baadhi ya klabu za nchini England tangu mwanzoni mwa mwaka huu, lakini mkazo wa viongozi wa Leicester City, ulikwamisha mpango huo.

Klabu za Man City, Man Utd, Chelsea pamoja na West Ham Utd zinatajwa kuwa katika mipango ya kumsajili mshambuliaji huyo, ambaye alimaliza msimu wa 2015-16 kwa kufunga mabao 24.

Hata hivyo Vardy, aliwahi kuweka wazi mustakabali wake wa soka, kwa kusema hafikirii kuihama klabu ya Leicester City, na badala yake amedhamiria kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha klabu hiyo ambayo iliushtua umma wa mashabiki wa soka duniani, kwa kupata mafanikio makubwa msimu uliopita.

Alvaro Morata Awachanganya Mashabiki Wa Juventus
Pep Guardiola Kuanza Na Ilkay Gundogan

Comments

comments