Waliokua mabingwa wa England msimu wa 2015/16 Leicester City, wamefanikisha usajili wa beki Harry Maguire akitokea Hull City.

Maguire mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano, huku akisajiliwa kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 17.

Licha ya Hull City kushuka daraja msimu wa 2016/17, Maguire alikuwa ni kati ya wachezaji wachache walioonyesha kiwango safi cha soka, ambapo mpaka pazia la ligi linafungwa alikuwa amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 36, hali iliyosababisha klabu kadhaa kuingia vitani kumsaka.

Maguire alijiunga na Hull City Julai 2014 akitokea Sheffield United kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 2.5 na kufanikiwa kucheza michezo sita tu kabla ya Februari 2015 kujiunga na Wigan Athletic kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Oscar Garcia Achukua Mikoba Ya Galtier - St Etienne
Jordan Pickford Aweka Rekodi Mpya England