Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, ameachiliwa na polisi nchini Kenya baada ya kukamatwa kwa madai ya kuingia nchini humo kinyume na sheria.

Kwa mujibu wa wakili wake, George Wajackoyah, Lema ambaye alikuwa ameambatana na familia yake alikua akielekea jijini Nairobi kwa ajili ya kutafuta makazi ya muda baada ya kutishiwa maisha.

Sasa mamlaka za Kenya zimemruhusu Lema na familia yake kubaki nchini humo wakati akiendelea na taratibu za kuwa mhamiaji wa muda.

Baada ya kuachiliwa, Lema amewaeleza wanahabari kwamba alitoroka Tanzania akihofia uhai wake baada ya kupokea vitisho bila ya kueleza vitisho hivyo vimetoka wapi.

Trump amtumbua Waziri wa Ulinzi
RPC Arusha: Lema yupo salama