Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema ameitikia wito wa Jeshi la polisi lililomtaka mapema leo kuripoti kituoni.

Sababu ya Lema kuitwa polisi bado haijawekwa wazi ila jana Oktoba 21, 2018 Lema alipigiwa simu na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’azi na kumtaka ajisalimishe.

Lema ameongozana na katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Elisa Mungure.

Jana kwenye ukurasa wa Twitter, Lema aliandika;

“Nimepigiwa simu na Polisi kwamba natakiwa kuripoti kituo kikuu cha Polisi Arusha leo bila kukosa, sijaelezwa sababu lakini wito unaonekana kuwa wa lazima sana, lakini nafikiri kupigania haki ndio linaweza kuwa kosa langu kubwa. MSIOGOPE,”amesema Lema

 

Babu Tale: Hawa hajakutwa na tatizo la ini, kama ilivyoripotiwa
Waziri Makamba kitanzini sakata la 'Mo Dewji' kutekwa

Comments

comments