Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema amemtaka Rais Dkt.  John Pombe Magufuli kuruhusu maandamano na kufanyika kwa shughuli mbalimbali za siasa.

Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Muriet Jijini Arusha, ambapo amemtaka Rais Dkt. Magufuli kuiga mfano wa Rais Uhuru Kenyatta wa kuruhusu maandamano kwa vyama vya upinzani.

Amesema kuwa kuruhusiwa kwa maandamano na mikutano ya kisiasa kuna faida ya pande zote mbili yaani upande wa chama tawala na upnde wa upinzani hivyo matokeo yake hunufaisha pande zote.

“Tunapaswa kujenga mfumo imara ili kiongozi yeyote akichaguliwa kuliongoza taifa hili, lazima afuate utaratibu huo ili kuendana na misingi iliyowekwa, lakini kwa sasa hatuna mfumo wowote ndio maana kila anayeingia anakuja na mfumo wake,”amesema Lema

Hata hivyo, akizungumzia sakata la shamba la Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye amesema kuwa ni uonevu na ukiukwaji wa utawala bora, kwani si kweli kuwa Sumaye hayaendelezi mashamba hayo.

 

Mbowe aonya kuhusu kauli za viongozi
Kagame kuiongoza Rwanda kwa muhula mwingine tena