Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limesema kuwa limefungua jalada la uchunguzi dhidi ya matukio ya vurugu zilizotokea katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kaloleni baada ya watu wawili kuchomwa kisu, huku mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akishushiwa kipigo.

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Ramadhan Ng’azi  amesema kuwa Lema ametoa taarifa hiyo ya kushambuliwa sambamba na mgombea udiwani wa kata hiyo, Boniface Kimario na wakala wake.

Amesema kuwa majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru wanakoendelea kupatiwa matibabu kutokana na majeraha waliyapata.

“Tumefungua jalada la uchunguzi dhidi ya watu waliohusika na tunawasaka, hakika watapatikana,”amesema Kamanda Ng’azi

Hata hivyo, katika jiji la Arusha unafanyika uchaguzi mdogo katika Kata nne kufuatia waliokuwa madiwani wa Chadema kujiuzulu na kujiunga na CCM.

 

Waziri Mkuu azindua uwanja wa kisasa wa mpira uliopewa jina lake
Kangi Lugola jino kwa jino na matapeli sekta ya michezo