Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema amekamatwa na Polisi baada ya Mahakama ya Wilaya ya Arumeru kumuachia huru

Mahakama ilimuachia huru Lema aliyekuwa anakabiliwa na kosa la uchochezi dhidi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kupeleka shahidi.

Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amethibitisha hilo na kusema kuwa Lema leo alihudhuria Mahakamani kwa ajili ya kesi iliyokuwa ikimkabili Lema.

“Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limemkamata Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwa kile kinachodaiwa “uchochezi”. Dhidi ya Mh Rais kuhusiana na ndoto aliyowahi kuota. Lema alihudhuria Mahakamani siku ya leo kwa ajili ya kesi iliyokua ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka 2 iliyopita. Baada ya Mahakama kufuta kesi hiyo leo na kuachiwa…Polisi walimkamata tena na kumfungulia kesi upya kwa mashtaka yale yale” amesema John Mrema

Kesi hii ni mwendelezo wa kesi iliyokua ikimkabili Mh Godbless Lema na ambayo ilimsotesha Mahabusu (Magereza) kwa zaidi ya miezi 4 mwaka juzi kabla ya kuachiwa kwa dhamana mapema mwaka jana.

RPC atolea ufafanuzi kuhusu kifo cha mdogo wake Heche
CCM yakomba safu nzima ya uongozi Chadema