Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewashangaa wanaomdhihaki na kumshambulia kwa manene makali mara baada ya kumpongeza mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu kufuatia kuwasaidia majeruhi wa ajali ya basi la Lucky Vicent.

Amesema kuwa kwa hapa nchini kuwa mpinzani wa siasa za bongo ni kazi ngumu sana, hivyo inahitaji kuwa na ujasiri wa kuweza kupambana ili uweze kushindana na kila anayekushambulia hata kwa lile jema unalolifanya.

Aidha, baada ya Mbunge Godbless Lema (Chadema) kumshukuru Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) Lazaro Nyalandu kuna kundi la watu liliibuka na kuanza kutoa maneno ya dhihaka kwa Lema huku wengine wakipongeza na kusema ni jambo la kheri kwa mbunge huyo kutambua kazi iliyofanywa na Nyalandu, lakini baada ya mijadala hiyo kuzidi kuwa mikuba Lema aliibuka na kutoa kauli hii kuwajibu waliokuwa wakimdhihaki.

“Kuwa mpinzani wa siasa Tanzania ni kazi ngumu sana, ila hatukati tamaa kwa sababu upendo wetu ni mkuu kuliko dhihaka. Mungu awabariki” aliandika Godbless Lema

 

Waziri Mkuu mgeni rasmi maadhimisho siku ya Albino
Matokeo sita katika mwili wako kama ukila ndizi 2 kila siku

Comments

comments